Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Sheikh Dr. Alhad Mussa Salum, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Maridhiano na Amani Tanzania (JMAT-TAIFA), anawatangazia na kuwaalika Waislamu wote pamoja na wananchi kwa ujumla kuhudhuria Hafla Kubwa na Tukufu ya Maulid ya Mtume Muhammad (saww) itakayofanyika Ijumaa, tarehe 17 Oktoba 2025, katika Masjid Majmuuat Al-Islaamiyyat - Temeke Mwisho, Dar es Salaam, mara baada ya Swala ya Isha.
Kwa mujibu wa Sheikh Dr. Alhad Mussa Salum, maandalizi yote yamekamilika kwa kiwango cha juu, na wageni mbalimbali wakiwemo viongozi wa serikali, taasisi za kidini, na wageni mashuhuri wanatarajiwa kuhudhuria.
Kaulimbiu ya mwaka huu:
“Tumuadhimishe Mtume (s) na Tufuate Nyayo Zake.”
Your Comment